Back to top

Mechi ya Kagera Sugar FC na Simba SC yaahirishwa.

18 December 2021
Share

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania(TPLB) imetoa taarifa ya kuahirishwa kwa mchezo namba 69 wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Kagera Sugar FC na Simba SC uliokuwa uchezwe Desemba 18, 2021 Saa 10:00 Alasiri katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, kutokana na taarifa za kitabibu kuwa wachezaji 16 kati ya 22 wa Simba SC waliosafiri kwenda Bukoba kuonekana kuwa na dalili ya mafua na kukohoa hali inayochangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa (Seasonal Influenza).