Mikoa sita ya Burundi inayopakana na Tanzania imesaini makubaliano na Mkoa wa Kigoma ili kuimarisha ulinzi na usalama baina ya pande mbili kutokana na mwingiliano wa wananchi wake kuhatarisha usalama wa nchi hizo na kuzorotesha mahusiano ya kijamii.
Katika zoezi hilo la utiaji saini Mkuu wa Mkoa wa Makamba Burundi ametia saini kwa upande wa Burundi na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye ametia saini kwa upande wa Mkoa wa Kigoma .