Back to top

MFUMO WA KIDIJITALI KWA JESHI LA ZIMAMOTO WAJA.

10 February 2022
Share

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto (SACF) Puyo Nzalayamisi amesema katika ziara ya Jeshi hilo kwenye vyombo vya habari vya IPP wamejifunza mambo lukuki ikiwemo kuzingatia muda katika utoaji wa taarifa hivyo kuahidi kuwa jeshi hilo litaboresha mfumo wa Kidijital utakaowezesha kutoa taarifa kwa wakati ili kutatua changamoto ya majanga ya moto, kwa kutambua kuwa mfumo wa kidijitali kwa sasa ndio ambao unaendeshwa kiulimwengu.
.
Katika ziara hiyo amekoshwa na vifaa vya kisasa vilivyopo ambavyo vinafanya kazi nyingi kwa wakati mmoja, sambamba na weledi wa hali katika kuzingatia taaluma ya habari kuhabarisha ulimwengu kwa habari zenye uhakika.
.
Amesema katika kuboresha mfumo huo watakuwa wanatengeneza video fupifupi zenye kutoa elimu ya majanga ya moto ili jamii ielewe juu ya madhara ya moto, ili pia kufanikisha hilo ameeleza kuwa watahakikisha wanawafikia watu mashuhuri ambao nikioo cha jamii ili wawe mabalozi katika kutoa elimu ya athari za majanga ya moto kwa jamii.