Back to top

MUHIMBILI YALAANI VIDEO YA PROF.JAY INAYOSAMBAA MTANDAONI AKIWA ICU.

10 March 2022
Share

Hospitali ya Taifa Muhimbili imelaani kitendo cha video iliyorekodiwa na kusambazwa mitandaoni ikimuonesha aliyekuwa Mbunge wa Mikumi(CHADEMA) na Msanii wa Bongo Fleva, Ndg.Joseph Haule (Profesa Jay) anayepokea matibabu hospitalini hapo akiwa ICU.ambapo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma Aminiel Aligaesha amesema kitendo hicho ni cha kukosa utu na maadili na kusema video hiyo haijarekodiwa na Hospitali hiyo.

Aligaesha amesema kuwa kutokana na kitendo hicho wanafuatilia na kuwasiliana na mamlaka husika ili kubaini chanzo cha video hiyo ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Ameongeza kuwa hospitali hiyo inahudumia wagonjwa takribani 3,400 kwa siku wakiwemo wananchi wakawaidia, viongozi wakuu wa serikali, wanasiasa na watu wengine kwa kuzingatia taaluma, utu na faragha.

Pia ametoa pole kwa mke wa Prof.Jay, familia na jamii nzima iliyoguswa na tukio hilo, na kuwaomba wananchi wanaotumia Hospitali ya Taifa Muhimbili, (Mloganzila & Upanga) kuendelea kuwa na imani na hospitali hiyo pamoja na kuheshimu taratibu za hospitali.