Back to top

CHONGOLO ATAKA MAKATIBU WILAYA KUSITISHA ZOEZI LA UPIGAJI KURA

21 April 2022
Share

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amewataka Makatibu wa Wilaya wa CCM nchini nzima kuhakikisha wanasitisha zoezi la kupiga kura na kurudisha zoezi la utoaji fomu kwenye sehemu ambazo zimeripotiwa kuwepo kwa matatizo ya wanachama kunyimwa fomu na Makatibu wa Matawi kwa kuficha fomu ikiwemo, Tandika, Manzese na Kimara huku wakitoa fomu kwa wale wanachama wa wanaodhani watalinda maslahi yao.  

Chongolo ametoa kauli hiyo kwenye ziara yake ya kutembelea matawi mbali mbali ya Chama cha Mapinduzi yaliyopo kwenye mkoa wa Dar es Salaam amesema katika zoezi la uchaguzi wa ndani unaoendelea kwenye chama hicho kumeibuka baadhi ya Makatibu wa Matawi wa chama hicho kuwafichua fomu baadhi ya wanachama wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi huku wakiwapatia fomu wanachama ambao wanaofikiri watalinda maslai yao suala ambalo amesema halikubaliki huku akiwataka Makatibu wa Wilaya nchi zima kurudisha zoezi la uchukuaji wa fomu na kusitisha upigaji wa kura maeneo yote yenye matatizo ikiwemo Tandika, Manzese, Kimara kwa lengo la kuwapatia haki ya kuchagua na kuchaguliwa sawa sawa na matakwa ya katiba ya chama hicho.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu Chongolo amesema kumeripotiwa kuwepo kwa baadhi ya maeneo ikiwemo Babati, Mbeya na Manyara pamoja na Wilaya ya Ubungo kuwepo kwa baadhi ya wagombea kuchukua kadi za CCM na kuwapatia watu ambao hawajahakikiwa kwenye kitabu cha uchaguzi wa chama hicho ambapo ametoa rai kwa Wakurugenzi wa uchaguzi kujiepusha kutumia vitabu vya majina yaliyoongozeka baada ya kuhakikiwa  kufanyka.