Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula ametoa onyo kwa viongozi wa Vijiji na Vitongoji kuacha mara moja kujivika madaraka na kuvunja sheria za ardhi, kugawa ardhi kinyume na sheria na kusababisha uvamizi kwenye maeneo yenye milki za watu wengine.
Dkt.Mabula ametoa onyo hilo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, wakati akitoa na kukabidhi taarifa ya uchunguzi wa migogoro ya ardhi katika eneo la Mapinga
Taarifa hiyo iliyokabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abuubakar Kunenge, inafuatia kuundwa kwa Kamati ya kuchunguza migogoro ya ardhi katika eneo la Mapinga wilayani Bagamoyo.
Katika taarifa yake ya uchunguzi kamati ilibaini mambo 11 yaliyochangia uwepo wa migogoro katika eneo la Mapinga ikiwemo viongozi kujivika madarala kinyume cha sheria kwa kugawa ardhi isivyo halali ambapo viongozi hao wamediriki kugawa hata maeneo yenye milki za watu wengine na kusababisha migogoro ya uvamizi.