Bodi ya Maziwa nchini, imewataka wenye viwanda vya kusindika maziwa, kuhakikisa wanatengeneza bidhaa zenye ubora ili kuleta ushindani wa soko, katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Wakizungumza katika kiwanda cha kusindika maziwa cha Tanga Fresh Jijini Tanga, viongozi wa bodi hiyo, wamesema ushidani wa bidhaa ya maziwa umekuwa mkubwa na kusababisha wasindikaji wa Kenya kuleta ushindani mkubwa dhidi ya Tanzania.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa wadau wa Bodi ya Maziwa waliotembelea kiwanda hicho, Bwana Ally Soro, amesema Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeweka kipaumbele zoezi la ufugaji ng'ombe bora wa maziwa ili kuongeza, upatikanaji wa maziwa.