Back to top

DAWASA MSILALE, MAJI NI HUDUMA NYETI - MAJALIWA

29 November 2022
Share

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) kuendelea kutafuta vyanzo vipya vya maji na kuviingiza kwenye mfumo huku akiwasisitiza wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kutambua kuwa maji ni huduma nyeti kwenye maisha ya binadamu hivyo wasilale bali waendelee kuwatumia wataalam wa ndani kutafuta maji zaidi.

“Ndugu wafanyakazi wa DAWASA mnapaswa kutambua maji ni huduma nyeti kwenye maisha ya binadamu, kazi yenu inahitaji uaminifu na uadilifu mkubwa, fanyeni kazi hii ya umma, wahudumieni watanzania, tambueni maeneo yenye uhitaji na mpeleke huduma” Waziri Mkuu - Kassim Majaliwa

Mhe.Majaliwa ameyasema hayo leo Novemba 29, 2022, alipotembelea eneo la mradi wa maji lililopo Kisarawe mjini, mkoani Pwani.