Back to top

MAGUGU MAJI ZIWA JIPE KUSHUGHULIKIWA

31 August 2023
Share

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.Selemani Jafo, amesema Serikali inaendelea na jitihada za kumaliza changamoto ya magugu maji kuzingira Ziwa Jipe wilayani Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro.

Amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mwanga Mhe.Joseph Tadayo, aliyetaka kujua lini Serikali itatekeleza mradi wa kuondoa magugu maji katika Ziwa Jipe.

Dkt.Jafo amesema Ofisi hiyo kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), tayari zimefanya tathimini ya uharibifu uliopo na kuandaa andiko la Mradi wa Hifadhi ya Ardhi, na vyanzo vya maji.

Ameeleza kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha inarejesha Ikolojia ya ziwa hilo ili kuleta manufaa kwa wananchi wanaozunguka eneo hilo pamoja na uhifadhi wa mazingira.