Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), imetangaza ongezeko la nauli Kwa mabasi ya mjini na mabasi ya masafa marefu, zitakazoanza kutumika kuanzia tarehe 08. 12. 2023.
Nauli hizo mpya zimetangazwa rasmi na Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, CPA Habibu Siluo wakati akizungumza jijini Arusha, na wamiliki wa usafirishaji kutoka mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.
LATRA imesema imeridhia kufanya marejeo ya nauli mpya za mabasi ya mijini na njia ndefu kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za gharama za uendeshaji kuwa kubwa na kuwafanya wafanyabiashara kushindwa kutoa huduma kwa uhakika.