
Bondia Tanzania Hassan Mwakinyo amesema atatumia pambano lake dhidi ya Muargentina Jose Carlos Paz litakalochezwa Novemba 13 kuwaonesha Watanzania kuwa hajaridhika na bado ana safari ndefu ya kufikia kilele cha mafanikio wakati atakapotetea mkanda wake wa WBF na kuwania mkanda mwingine wa I.B.A.
Bondia huyo ameahidi makubwa kwa mashabiki wake kwa kucheza mchezo tofauti ambao wengi bado hawajawahi kushuhudia akiucheza.