Back to top

AFARIKI BAADA YA KUCHOMWA MOTO NA MCHUMBA

05 September 2024
Share

Mwanariadha wa Uganda Rebecca Cheptegei (33), ambaye alikuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi nchini Kenya, baada ya kuchomwa moto na mpenzi wake Dickson Ndiema amefariki.

Tukio hilo la limetokea siku ya Jumapili katika mji wa Endebess Magharibi ya Kenya, ambapo kwa mujibu wa ripoti ya polisi, inasema Rebecca alimwagiwa petroli na mpenzi wake na kisha kumchoma moto. 

Rebecca Cheptegei alikuwa amepata majeraha asilimia 80 ,  kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa madaktari katika Hospitali ya Rufa na mafunzo na Moi (MTRH) mjini Eldoret nchini Kenya.

Mauaji hayo yametokea wiki kadhaa baada ya Cheptegei kushiriki katika mashindano ya olimpiki jijini Paris, ambapo alimaliza katika nafasi ya 44 kwenye mbio za masafa marefu.

Vyombo vya habari nchini Kenya, vimeeleza kwamba mmoja wa watoto wa kike wa Rebecca Cheptegei alishuhudia tukio hilo.