Back to top

VIJANA WANNE WAKOSOAJI WALIOTEKWA KENYA WAMEPATIKANA

06 January 2025
Share

Vijana wanne wakosoaji wakuu wa Rais William Ruto kwenye mtandao wa kijamii kati ya 6 wanaoaminika kutekwa nyara na vitengo vya usalama nchini Kenya wamepatikana wakiwa wametupwa maeneo mbalimbali nchini Kenya.

Billy Mwangi, Mwanafunzi wa Chuo aliyetoweka baada ya kutekwa nyara na wanaume wanne waliovalia barakoa katika mji wa Embu, amepatikana akiwa hai Kaunti ya Embu, na baada ya kufika nyumbani kwao Jumatatu asubuhi alipelekwa hospitalini kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 24, alitekwa na watu wasiojulikana alipokuwa akisubiri kuhudumiwa kwa kinyozi katika mji wa Embu Jumamosi, Desemba 21.

Kijana wa pili aliyetoweka Benard Kavuli aliyetekwa nyara mnamo Desemba 22, katika eneo la Ngong akipatikana eneo la Moi’s Bridge Kaunti ya Trans Nzoia kilomita 400 kutoka eneo alikotekwa.

Peter Muteti  aliyetekwa katika eneo la Uthiru mnano Desemba 21 akipatikana katikati mwa Jiji la Nairobi mapema hii leo.

Kijana wa tatu Ronny Kiplagat ambaye pia nduguye Yoko Kibet almaarufu Kibet Bull alipatikana Kaunti ya Machakos baada ya kutekwa mnano Desemba 25 katika eneo la Kikuyu Kaunti ya Kiambu, hata hivyo nduguye Yoko Kibet ambaye ni mchoraji vibonzo hajaachiwa.


Hata hivyo, Steve Mbisi aliyetoweka eneo la Mlolongo Desemba 17 hajulikani aliko.

Maafisa wa Polisi hata hivyo wamekanusha kuhusika na utekaji huo, ambao umezua hisia kali nchini Kenya hata hivyo vijana hao waliopatikana walionekana wadhaifu na waliochanganyikiwa.