Back to top

Ajali ya basi na Treni yaua 10 Kigoma

06 June 2018
Share


Watu 10 wamefariki pap hapo na wengine 26 wamejeruhiwa katika ajali ya Basi la kampuni ya HAMIDA lililokuwa likisafiri kutoka Kigoma kwenda Nzega mkoani Tabora kugonga treni ya mizigo katika makutano ya barabara na Reli eneo la Gungu mjini Kigoma.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma Martin Otieno amesema ajali hiyo imetokana na uzembe wa dereva na mwendo kasi kwa sababu treni ilitoa ishara zote zinazopaswa kabla ya kupita eneo hilo.

Hata hivyo amesema kati ya majeruhi hao wengine walikuwa kando ya barabara na idadi inaweza kuongezeka kutokana na hali waliokuwa na hayo.

Tayari maiti zimepelekwa kuhifadhiwa katika chumba cha maiti hospitali ya mkoa wa Kigoma Maweni pamoja na majeruhi 28 ambao wamelazwa na kuanza kupatiwa matibabu.