Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, David Concar amesema kuwa Maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi wanapaswa kuwa makini na uwasilishwaji wa taarifa kwa umma ili kuepuka baadhi ya watu wengine kuzibadilisha taarifa kwa lengo la kupotosha wananchi wakati wa majanga na dharura.
Balozi David Concar amesama hayo wakati akufunga mafunzo awamu ya pili ya kuwajengea uwezo wa mawasiliano maafisa wa Jeshi hilo wakati wa majanga na dharura yaliyofanyika jijini Dar es salaam.
Kwa upande wake Kamishina wa Intelijensia ya makosa ya Jinai CP Charles Mkumbo amewataka washiriki kutumia mafuzo hayo vizuri ambapo yatawajengea uwezo mkubwa wa kutoa taarifa zinazozingatia vigezo ili kuepuka kutoa taarifa za upotosha katika jamii.