Benki Kuu ya Tanzania imehamisha mali na madeni yote ya benki M kwenda benki ya Azania Limited baada ya benki hiyo kushindwa kujiendesha.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt.Benard Kibese amesema benki M ilipewa zaidi ya miezi sita ijiendeshe kwa mujibu wa taratibu lakini ilishindwa kufanya hivyo.
Amesema kinachoendelea kwa sasa ni kukamilishwa kisheria ili uhamisho huo uweze kukamilika kama unavyopaswa.