Back to top

Bilioni 105 zatengwa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali 67 za wilaya.

13 August 2018
Share

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe Suleiman Jafo amewaagiza waganga wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia vyema rasilimali fedha, madawa pamoja na vifaa tiba katika maeneo yao ili zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa huku akidai kuwa serikali imetenga Bilioni 105 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali 67 za wilaya katika maeneo mbalimbali ili kuwaondolewa wananchi adha ya kupata huduma ya afya.

Akizungumza  jijini Dodoma na waganga wakuu wa mikoa na wilaya nchi nzima Waziri Mhe Jafo amesema yapo maeneo ambayo hamna hospitali ya wilaya ambapo katika mwaka huu wa fedha maeneo hayo yatajengewa hospitali ambapo amewataka wataalamu hao kusimamia sekta ya afya kikamilifu.

Akitoa salamu kwa Niaba ya Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Katibu Mkuu wa wizara hiyo dr mpoki ulisubisya amesema ili tanzania kufikia uchumi wa kati kuna kila sababu ya kuimarisha sekta ya afya kwa kujenga viwanda kutengeneza dawa na vifaa tiba.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa waganga wakuu wa mikoa Dr Grace Maghembe amesema wanaendelea na jitihada mbalimbali za kukabiliana na magonjwa ya milipuko ikiwemo ugonjwa wa kipindupindu kwa kushirikiana na sekta mbalimbali ikiwemo wizara ya maji na umwagiliaji.