Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Bw. Daniel Chongolo, amewataka vijana mkoani humo kuacha kushawishika na kutumiwa na baadhi ya watu wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi, hasa kuelekekea kipindi cha uchaguzi kwani vitendo hivyo vitasababisha kupata viongozi wasiokuwa na sifa.
Bw. Chongolo amayasema hayo wakati akizungumza na makundi mbalimbali ya vijana mkoani humo, wakiwemo Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), ambapo ameongeza kuwa hivi karibuni wameonekana baadhi ya vijana wakitenegeza sifa kwa viongozi wasio na dhamana, ili waonekane kuwa na sifa ambapo amesema kazi ya jumuiya hiyo ya vijana sio upambe.
Aidha Chongolo, ameongeza kuwa kazi ya vijana wanaounda jumuiya hiyo ya UVCCM ni kuhakikisha wanalinda Katiba ya Chama Cha Mapinduzi, kulinda kanuni inayolinda umoja huo pamoja na kuwalinda viongozi wanaopatikana kihalali.