Mamlaka ya Nafaka na Mazao mchanganyiko (COPRA), Imeingia makubaliano na taasisi zinazohusiana na usambazaji, usindikaji na uchakataji wa zao la ngano nchini ambayo yatakwenda kuongeza chachu ya uzalishaji wa zao la hilo hapa nchini.
Wamesaini makubaliano hayo na Mkurungenzi wa Mamlaka hiyo Bi. Irene Mlola katika viwanja wa Nane nane Nzuguni jijini Dodoma, na kushuhudiwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde.
Akizungumza katika hafla Hiyo Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde Ameipongeza COPRA kwa kusaini makubaliano hayo na kusema hatua hii ni chachu ya wakulima kuchangamkia fursa ya uzalishaji kwa kuwa soko lipo la uhakika.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa COPRA Bi. Irene Mlola ametoa rai kwa wakulima hapa nchini kuzalisha ngano kwa wingi na yenye ubora ili kampuni hizo ziweze kupata ngano ya kutosha ili kukizi Soko la ushindani.