Mkuu wa Jeshi la polisi nchini (IGP), Simon Sirro amekutana na kuzungumza na wakazi wa eneo la mpaka wa Tanzania na Msumbiji mkoani Mtwara ambapo kulitokea mauaji ya watanzania 9 na wengine kujeruhiwa June 26.
Ambapo IGP Sirro amesema ameongea na IGP wa Msumbiji ambapo amemuomba kesho June 30 wakutane kuongea nae juu ya tukio hili.
IGP Sirro amewasihi Watanzania wanaofanya shughuli za kilimo Msumbiji kusitisha shughuli hizo kwa muda mpaka hali itakapo kuwa shwari na amesema wameongeza askari wengi katika eneo la mpakani mwa Msumbiji na Tanzania kwaajili usalama zaidi.
Amesema watatoa zawadi nono kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa wahalifu hao.
kutokana na taarifa ya diwani wa kata ya Kitaya wanawake watatu na mtoto mmoja bado hawajapatikana hadi sasa tangu kutoa kwa tukio hilo ambapo IGP Sirro amesema watapambana kuhakikisha wanapatikana.