Back to top

Jafo asema awamu ya 3 ya Nyungu na kujifukiza inaanza Februari 01.

30 January 2021
Share

Waziri wa TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo amesema Corona haina nafasi kwa nchi ya Tanzania hivyo kuanzia February 01 hadi February 07, 2021 awamu ya tatu yaani (Season Three) ya nyungu, kujifukiza, kula matunda na kumuomba mungu itaanza.

"Rais Magufuli juzi ulisema Watanzania tuko salama, angalia Umati huu wote tuko salama, hapa Corona haina nafasi, tutaendelea  kumuomba Mungu na umesema Watu wajifukize sana, Jumatatu tunaanza Kampeni nyingine ya Wiki moja 'Season' 3 , nyungu kama kawaida"-Jafo - TAMISEMI.

Waziri huyo wa TAMISEMI ameyazungumza hayo wakati wa shughuli ya kuwekwa jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli.