Back to top

Jiji la Dodoma latahadharisha ununuzi wa ardhi kiholela

02 July 2018
Share

Halmashauri ya Jiji la Dodoma imewatahadharisha wananchi kuepuka kununua ardhi kiholela kwa kisingizio cha kuchangamkia fursa ya ujio wa makao makuu ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima wakati huu ambapo tayari ramani ya mpango kabambe wa ujenzi wa mji wa kisasa wa serikali ikiwa imekamilika.

Mkurugenzi mtendaji wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi anasema mpango huo umezingatia matumizi bora ya ardhi ikiwemo ujenzi wa mji wa  serikali, maeneo tengefu ya viwanda ,shughuli za kijamii na makazi huku akiwataka wananchi kufuata taratibu kwenye ununuzi wa ardhi.

Kuhusu utunzaji wa mazingira na usafi katika jiji hilo jipya mstahiki meya wa Jiji Profesa Davies Mwamfupe anasema suala hilo ni mtambuka na kila mtu anapaswa kufahamu umuhimu wake huku akionya hatua kali zitachukuliwa kwa wananchi watakaokiuka kanuni za usafi na utunzaji mazingira.

Katika hatua nyingine Jiji hilo limesaini mkataba wa makubaliano ya kuboresha mandhari na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ambapo mamlaka hiyo itatunza mizunguko iliyopo kwenye barabara za jiji hilo pamoja kutangaza utalii na vivutio vilivyopo Dodoma.