Halmashauri ya wilaya ya Singida imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni 92 kutokana na mapato yatokanayo na mifugo,ambapo baadhi ya fedha hizo zimetumika kukarabati majosho na kununua madawa kwa ajili ya kuogeshea mifugo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Singida Bwana Rashidi Mandowa amesema hayo wakati wa kuogesha mifugo ambayo madawa yake yametolewa na serekali na kusema kuwa moja ya mapato makubwa yanayotegemewa na halmashauri yake ni mapato yatokanayo na mifugo.