
Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania JWTZ kupitia shule ya mafunzo ya awali ya kijeshi ya RTS Kihangaiko limeanza kutekeleza mpango maalum wa kuwaandikisha jeshini moja kwa moja kutoka shuleni wanafunzi waliomaliza kidato cha sita na kufanya vizuri kwenye masomo ya sayansi lengo likiwa ni Tanzania kupata askari wasomi wenye uwezo mkubwa wa kiteknolojia watakaoweza kukabiliana na wahalifu na ugaidi wenye teknolojia ya juu ambao unaendelea kwa kasi kubwa duniani
Mkuu wa shule ya mafunzo ya awali ya kijeshi RTS Kihangaiko Kanali Sijaona Myala ametoa kauli hiyo katika hitimisho la mafunzo ya matumizi ya silaha za kivita kwa askari wanafunzi zaidi ya mia nne yaliyofanyika katika eneo la vilima saba Msata wilayani Bagamoyo.
Mkuu wa mafunzo ya kivita makao makuu ya jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania Brigedia Generali Deodatus Kanyata anasema jeshi lina wajibu mkubwa wa kuhakikisha rasilimali zote za nchi zinakuwa salama wakati wote kwa manufaa ya taifa hivyo kuna muhimu wa kuwa na jeshi la kisasa lenye wasomi.
Wakufunzi wa shule ya mafunzo ya awali ya kijeshi ya RTS Kihangaiko nao wapata nafasi ya kutoa nasaha ka vijana wanaojiunga na jeshi hilo.