Back to top

Kabuga mtuhumiwa mauaji ya kimbari akana kufadhili mauaji hayo.

28 May 2020
Share

Mtuhumiwa mkuu wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda Félicien Kabuga anayetuhumiwa kwa kufadhili wa mauaji hayo amekanusha madai hayo.

"Huo wote ni uongo, Sikumuua Mtutsi yeyote, nilikuwa nafanya nao kazi," 

Félicien Kabuga aliiambia Mahakama ya Ufaransa wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake.

Mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 84 alikamatwa mapema mwezi huu viungani mwa mji wa Paris baada ya kutafutwa kwa miaka 26.

Bwana Kabuga anadaiwa kuwafadhili silaha jamii ya kihutu ambao waliwauwa watu wapatao 800,000 mwaka 1994.

Kwa zaidi ya siku 100, mauaji hayo yalilenga jamii ya kabila la Watutsi ambao walikuwa wachache na wapinzani wao wa kisiasa bila kujali asili ya kabila lao.

Chapisho lililopita Link https://www.itv.co.tz/news/kabuga-mtuhumiwa-wa-mauaji-ya-kimbari-rwanda-kufikishwa-mahakamani