Back to top

Mahakama kuu ya Tanzania imebatilisha sheria ya uchaguzi.

10 May 2019
Share

Mahakama kuu ya Tanzania imebatilisha sheria inayowapa mamlaka wakurugenzi wa halmashauri na manispaa kusimamia uchaguzi mkuu hapa nchini.

Uamuzi huo umetolewa na Kaji Atuganile Ngwala katika kesi ya msingi namba 6 ya mwaka 2018 iliyofunguliwa na mtoto wa marehemu Chacha Wangwe ambaye ni Bob Chacha Wangwe.

Katika kesi hiyo ya kikatiba, Jaji Ngwala amebatilisha vifungu viwili vya katiba cha 7 (1) ambapo kinaeleza kuwa 'kila mkurugenzi wa jiji na halmashauri wanakuwa wasimamizi wa uchaguzi mkuu.

Jaji ngwala amesema jambo hilo haliwezekani kwa sababu wakurugenzi wanateuliwa na rais, hivyo hawachaguliwi kupitia mfumo wa tume ambapo watu wamekuwa wakilalamika kuhusu tume huru ya uchaguzi.

Pia imebatilisha kifungu cha 7 (3) kinachoeleza kuwa tume inaweza kumchagua mtu yoyote kuwa msimamizi wa uchaguzi wakati katiba inasema huwezi kuwa mwanasiasa na ukawa msimamizi wa uchaguzi bali inatakiwa achaguliwe mtu huru.

Baada ya kueleza hayo, jaji ngwala amesema anazifuta sheria hizo na kama kuna upande haujaridhika ukate rufaa.

Licha ya hukumu hiyo kutolewa upande wa serikali mpaka sasa haujasema kama utakataa rufaa kuhusiana na uamuzi huo wa mahakama.