Back to top

MAKANDARASI WAZAWA WAPIGIWA DEBE, KOREA.

09 September 2024
Share

Waziri wa Ujenzi Mh.Innocent Bashungwa, ametoa wito kwa makampuni ya ujenzi ya Korea, kushirikiana na Makandarasi wazawa wa nchini Tanzania katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi ambayo itawawezesha Makandarasi wazawa kujengewa uwezo na kupata ujuzi wa teknolojia za ujenzi wa miundombinu.

Waziri Bashungwa ametoa wito huo, walipokutana na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Fedha ya Korea inayoshughulika na  Ujenzi (K-FINCO), Dk. Lee Eun Jae pamoja na Watendaji wakuu wa Makampuni Makubwa ya Ujenzi zaidi ya 30 ya Korea Kusini, huko jijini Seoul, Korea Kusini.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Fedha ya Korea, kwa ajili ya Ujenzi (K-FINCO), Dkt. Lee Eun Jae ameeleza kuwa Serikali ya Korea itaendelea kushirikiana na Tanzania ambapo tayari wameshafanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kusaini hati za makubaliano na Wizara ya Ujenzi na Taasisi mbalimbali ikiwemo Benki ya NMB.