
Mke wa Rais mama Janeth Magufuli ameguswa na kutoa msaada wa vyakula vya aina mbalimbali kwa wafungwa wa gereza la Ukonga huku akiwataka watanzania kuondokana na dhana potofu kuwa wafungwa walioko magerezani ni wahalifu na kwamba nao kama binadamu wengine wanahitaji misaada na faraja.
Akizungumza na baadhi ya maafisa wa magereza waliofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuupokea msaada huo kwa niaba ya wafungwa wa gereza hilo mama Janeth Magufuli amesema ni jukumu la kila mmoja wetu kuwasaidia watu wasiojiweza wakiwemo wafungwa wa magerezani.
Mama Janeth Magufuli amekabidhi mchele tani tani nne nukta nane,unga wa mahindi tani nne nukta nane,sukari tani mbili nukta nane pamoja na tende huku akiwatakiwa waislamu wote nchini mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa ramadhani na kuwataka katika kipindi hiki cha mfungo mtukufu wa ramadhani kuliombea taifa amani.
Kwa upande wake Kamishna Gaston Kalam Sanga Kaimu Kamishna mkuu wa magereza amemshukuru mama Janeth Magufuli kwa msaada huo na kutoa wito kwa wakuu wa magereza kunakopelekwa msaada huo kuhakikisha msaada huo unawafikia wahusika na si vinginevyo.