Ukosefu wa mashine za kuchapa na kudurufu maandishi ya nukta nundu kwaajili ya kuandaa mitihani ya majaribio kwa wanafunzi wenye ulemavu wasioona kumetajwa kudumaza juhudi za wanafunzi wenye ulemavu kufanya vizuri kwenye mitihani ya mwisho ya kihitimu darasa la saba hali iliyowalazimu wadau wa elimu mkoa wa Arusha kuanza kujitolea kwa hali na mali kumaliza changamoto hiyo.
Akizungumza na wadau wa elimu wazazi wanafunzi wenye ulemavu na baadhi ya viongozi wa serikali katika harambee ya kuchangia ununuzi wa mashine za kuchapa maandishi ya a nukta nundu Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya wenye ulemavu mkoa wa Arusha Saidi Kabende anasema tatizo ilo limechangia wanafunzi wenye ulemavu wa macho kushindwa kufanya vizuri kwenye mitihani ya mwisho.
Akiongoza harambee hiyo iliyofanyika katika shule ya msingi Upendo mkuu wa wilaya ya Arusha Fabiani Dakaro ameitaka jamii kushirikiana na serikali kutatua changamoto zinazowakabili watoto wenye ulemavu.