Upepo mkali uliokuwa unavuma eneo la kusini magharibi mwa fukwe ya Cornwall nchini Uingereza umeikokota meli ya mizigo ya Urusi ya Kuzma Minin na kuipeleka ufukweni na hivyo kushindwa kuendelea na safari mapema alfajiri hii leo.
Kitengo cha huduma za dharura za uokozi nchini Uingereza kimeanza jitihada za kuinasua meli hiyo iweze kuendelea na safari yake.
Taarifa zinasema kuwa ndani ya meli hiyo ya mizigo kuna wafanyakazi wasiopungua 18 na kwamba haikuwa imebeba mzigo ndani yake.