Waziri wa Viwanda na Biashara,Mhe Dkt. Ashatu Kijaji, amesema Serikali inaendelea na mchakato wa kuandaa mfumo mmoja wa ukusanyaji wa kodi kwa wafanyabiashara nchini, ili kuondoa kero ya taasisi mbalimbali za Serikali kukusanya kodi.
Ametoa kauli hiyo Jijini Mbeya wakati wa Mkutano wa Majadiliano kati ya Sekta Umma na Sekta binafsi, uliokuwa na lengo la kujadiliana namna ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara katika Mkoa huo.
Dkt.Kijaji amesema kero hiyo imekuwa ikilalamikiwa kwa muda mrefu na wafanyabiashara pamoja na wadau mbalimbali kuwa ilikuwa ikichangia kuua biashara na kufukuza wajasiriamali.