Back to top

Miaka 56 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

26 April 2020
Share

Watanzania leo wanaadhimisha kumbukumbu ya miaka 56 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa na hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na hayati Abeid Amani Karume.

Viongozi hao wawili walichanyanya mchanga wa pande hizo mbili kuashiria kuungana kwa Zanzibar na Tanganyika.

Taifa linaadhimisha kumbukumbu hiyo bila ya sherhe zozote baada ya kufutwa na Rais Dakta John Pombe Magufuli kutokana na kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona kwa kuepuka mikusanyiko.

Rais Magufuli ameamuru Shilingi Milioni 500 zilizotengwa kwa ajili ya sherehe za muungano zipelekwe kwenye mfuko maalum wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupambana na janga la Corona.

Uongozi wa ITV/Radio One unawatakia maadhimisho mema ya Muungano na kuwahimiza kufuata masharti ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona.