Back to top

Mikoa ya Singida na Dodoma yaagizwa kutumia tafiti za Kilimo.

05 August 2019
Share

Serikali imeiagiza mikoa ya Dodoma na Singida kutumia tafiti mbalimbali ili kuboresha kilimo huku ikisisitiza kwamba bila kutumia mbegu bora wakulima hawawezi kuzalisha mazao yenye tija.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo akizungumza katika uzinduzi wa maonesho ya nane nane kanda ya kati jijini Dodoma na kutaka maonesho hayo yawe na umuhimu mkubwa hususani kwa wakulima, wavuvi na wafugaji ambao wamekuwa wakipata elimu mbalimbali katika kuboresha sekta hiyo.

Awali mkuu wa mikoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge akimkaribisha Waziri amesema kuwepo kwa tatizo la masoko katika bidhaa zinazo tokana na kilimo, ufugaji na uvuvuvi jambo ambalo serikali haina budi kuwasaidia wakulima ili kuongeza hamasa kwa wananchi wengi kuwekeza zaidi katika sekta muhimu ya kilimo.

Nao baadhi ya washiriki wa maonesho hayo wamewaomba wananchi kujitokeza katika maonesho hayo kwa lengo la kujifunza teknolojia mbalimbali za kilimo.