Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Luten Jenerali Yakubu Mohamed amesema Jeshi ilo halitamvumilia askari wa jeshi ilo atakaye kiuka taratibu na kanuni za kijeshi ikiwemo kujihusisha na masuala ya kisiasa pamoja na utovu wa nidhamu hatua kali ikiwemo kufutwa kazi zitachukuliwa kwa watakaobainika kutenda hayo.
Mnadhimu Mkuu wa majeshi ya ulinzi ya wananchi wa Tanzania ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na zaidi ya askari wanafunzi elfu mbili kundi la 38 A wakiyohitimu mafunzo ya awali ya kijeshi katika shule ya mafunzo ya awali ya kijeshi ya RTS Kihangaiko iliyopo Msata wilayani Bagamoyo.
Kaimu Mkuu wa shule ya mafunzo ya kijeshi ya RTS Kihangaiko Kanali Sijaona Myala amesema askari hao wamepata mafunzo ya kutosha yanayowawezesha kufanyakazi kwa weledi wa hali ya juu katika ulinzi wa tTanzania na watu wake.
Katika shughuli hiyo pia askari wapya kutoka kabila la Wahadzabe walipata nafasi ya kutumbuza wimbo unaoishukuru serikali kwa kuwapatia nafasi maalum kwao ya kujiunga na jeshi ilo.