Back to top

MNH YAPOKEA VIFAA TIBA KUSAIDIA AFYA YA AKILI

23 April 2025
Share

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa vifaa tiba na kufundishia kutoka Al Muntazir Islamic International School, lengo ni kuboresha huduma kwa watu wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali za afya ya akili katika hospitali hiyo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo mshauri wa shule (school counsellor), Sayyida Tehsin amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa afya ya akili hasa kwa watoto na vijana, shule hiyo iliona ni vyema kutoa mchango wao ili kusaidia kuwapa faraja na matumaini wagonjwa wa afya ya akili waliopo MNH.

Aidha, wanafunzi wa shule hiyo walioshiriki katika kukabidhi msaada huo walipewa elimu ya afya ya akili na wataalamu kutoka MNH, ikiwa imelenga kuwajengea uelewa juu ya umuhimu wa afya ya akili, namna ya kutambua viashiria vya matatizo ya kiakili, na jinsi ya kusaidia wenzao wanaokumbwa na changamoto hizo. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Afya ya Akili kutoka MNH, Dkt. Praxeda Swai ameshukuru uongozi wa shule hiyo pamoja na wanafunzi kwa kujitoa kwao kusaidia jamii, akisisitiza kuwa msaada huo utasaidia kuboresha mazingira ya matibabu na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.