Back to top

Morogoro yaongoza kwa idadi kubwa ya wagonjwa wa ukoma.

18 January 2019
Share

Mkoa wa Morogoro umeendelea kuongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa ukoma kati ya mikoa tisa inayokabiliwa na ugonjwa huo hapa nchini.

Mwakilishi wa shirika lisilo la kiserikali la German Leprosy and Tuberculosis Relief Association la nchini Ujerumani  Burchad Lwantoga, amesema hayo mjini morogoro na kubainisha kuwau wameendelea kusaidia wagonjwa na kuhamasisha jamii juu ya dalili na athari zinazotokana na ugonjwa huo.