Marais na Mawaziri Wakuu wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameeleza kuridhishwa na utekelezaji wa mradi mkubwa wa kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere Huku wakishauri wananchi kufuata maelekezo ya wataalamu katika kutumia maji yatakayoingia kujaza bwawa hilo na yale watakayopata baada ya kuzalisha umeme.
Viongozi waliotembelea ni pamoja na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Jakaya Kikwete, Mawaziri Wakuu wastaafu Cleopa Msuya,John Malecela na Mizengo Pinda.