Back to top

MTAMA: MAMA SAMIA LEGAL AID YATATUA MIGOGORO 27 KATI YA 32

21 February 2025
Share

Migogoro  27 kati ya  32 imetatuliwa  kupitia Kampeni  ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Legal Aid. 

Akizungumza na Wananchi wa Mnolela  Ijumaa Februari 21,2025  Mratibu wa Kampeni ya Msaada ya Kisheria ya Mama Samia Wakili  Rockus  Komba amesema kuwa wamefanya mikutano katika vijiji sita na kuweza kutatua migogoro  ikiwemo migogoro ya Ardhi pamoja na familia.

Amesema kuwa, Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia inasaidia sana kwa Wananchi ambao hawawezi kuwafikia Wanasheria kutokana na kukosekana kwa uwezo wa kifedha.

"Hadi sasa tumeshatatu migogoro 27 kati ya 32 tumeshapatia ufumbuzi ,na iliyobakia tumeshaipeleka sehemu husika ili kupata ufumbuzi naamini hadi tutakapo maliza Kampeni hii tutakuwa tumemaliza maeneo migogoro yote ya Halmashauri ya Mtama."Amesema.Wakili  Komba

Naye Mkuu wa dawati la Jinsia na Watoto Joyce Kitesho alipokuwa anatoa elimu ya unyanyasaji wa kijinsia na migogoro ya ndoa amewataka wanawake wasifumbie macho ukatili wa aina yoyote ambao unaweza kuhatarisha maisha yao

"Wanawake wenzangu nawaomba msifumbie macho maswala ya unyanyasaji majumbani kwetu tutoe taarifa  tusifumbie macho,
Amesema Katesho.

Wananchi wa Mnolela wameishukuru Serikali kwa kuwaletea msaada wa kisheria katika maeneo yao kwani itasaidia sana kuondoa migogoro mingi ambayo inatokea kila wakati kwenye jamii zao.

Zabibu  Saidi mkazi wa Mnolela,amesema kuja kwa  Kampeni ya Mama Samia itasaidia kuondoa changamoto za migogoro katika maeneo yao na kuweza kuleta suluhu katika jamii.

"Kampeni ya Msaada wa Kisheria utasaidia kwa sisi Wananchi wa Lindi kupunguza migogoro ambayo inatokea kila wakati kwenye maeneo yetu, kama  migogoro ya Ndoa. Nimefurahi sana kuona ipo kwenye orodha kwani Wanandoa wengi wananyanyasika majumbani" Amesema Said.