Mkazi wa kitongoji cha Sindika kilichoko kwenye kata ya wilayani Karagwe mkoani Kagera, Daud Rwegasira anadaiwa kuuawa na ameuawa mgambo wawili wakati akijaribu kuwazuia mgambo hao wasimkamate Theopil Pima anayetuhumiwa kuwa amedhulumu pesa aliyopewa kwa ajili ya kununua kahawa.
Kamanda wa polisi mkoani Kagera kamishina msaidizi Revocatus Malimi akizungumza na waandishi wa habari ametaja majina ya watuhumiwa hao ambao kwa sasa wanashikiliwa na polisi kuwa ni Jackson Boneventura na Paul Berebera.
Kamanda huyo amesema upelelezi wa kesi hiyo unaendelea na ukikamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani .