Back to top

NAIBU WAZIRI PINDA AITAKA NHC KUJENGA NYUMBA ZENYE UHITAJI MIJINI

25 October 2024
Share

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda, amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kujenga nyumba zenye uhitaji katika maeneo ya mijini.

Mhe. Pinda ametoa kauli hiyo tarehe 24 Oktoba 2024 jijini Arusha wakati akikabidhi hati milki za ardhi kwa wananchi walionunua viwanja kupitia Mradi wa Safari City unaotekelezwa na Shirila la Nyumba la Taifa (NHC).

Amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kutouza nyumba zilizopo kati kati ya miji na badala yake wazibomoe na kujenga upya kulingana na uhitaji wa maeneo husika.

Kwa upande wake Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Arusha Bw. Benit Masika amesema, shirika lake hadi sasa limeweza kuuza jumla ya viwanja 1,026 ambapo kati ya hivyo viwanja 350 wateja wake wamemaliza malipo kwa asilimia 100.

Mradi wa Safari City ulioandaliwa eneo la ekari 587 katika mpango kabambe wa mwaka 2014 upo eneo la Burka Mateves ndani ya jiji la Arusha. Mradi huo una jumla ya viwanja 1913 kwa ajili ya uendelezaji wa nyumba za makazi, majengo ya biashara, huduma za jamii kama vile shule, vyuo, hospitali, sehemu za ibada, sehemu za michezo, kupumzikia na maeneo ya usalama wa miji kama vituo vya polisi, zimamoto na maeneo ya viwanda vido vidogo.