Back to top

Ndugai ahoji kitendo cha Zitto kuandika barua World Bank.

31 January 2020
Share

Spika wa Bunge Mhe.Job Ndugai amehoji kitendo kilichofanywa na mbunge wa Kigoma Mjini Mhe.Zitto Kabwe cha kuandika barua kwenda World Bank nchi  ikose  mkopo wa kuboresha elimu.

Mhe Ndugai amezungumza bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu yaliyolengwa katika Sekta ya Elimu ambapo amesema jambo hilo ni kwenda mbali mno na kwamba wanasubiri ufafanuzi wa Mhe.Zitto Kabwe atakaporejea bungeni.

"Waheshimiwa Wabunge wakati mwingine mwenendo wetu unakuwa haueleweki kwa mfano Mbunge mwenzetu atakaporudi labda anaweza akatufafanulia Mhe Zitto Kabwe kuandika barua World Bank kwamba nchi yetu ikose fursa ya mkopo ambao lengo lake ni elimu,kwasababu ya tofauti za sera ambazo ni jambo la kawaida..lakini kufikia mahali na ku-block Tanzania isipate fursa fulani nadhani ni kwenda mbali mno,Sijui katika hilo kama mbunge unafaidika nini".Job Ndugai.