Back to top

"NISHATI SAFI YA KUPIKIA INA FAIDA NYINGI KIAFYA" KAPINGA

08 September 2024
Share

Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia. 

Mhe. Kapinga  ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam, wakati wa Tamasha la Azimio la Kizimkazi, ambalo limetumika kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia likihusisha Mamalishe na Babalishe Jijini Dar es Salaam. 

"Kiongozi aina ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ana maono ya nishati safi ya kupikia hapatikani mara zote, hatokei mara zote hivyo tuna wajibu wa kumuunga mkono katika ajenda hii ambayo faida zake ni nyingi kiafya, kimazingira, kiuchumi na kijamii." Naibu Waziri Kapinga
 
Ameongeza kuwa,  Rais Samia amesimamia maono yake na kuwafanya Watanzania, Afrika na Duniani kote kusimama pamoja naye katika matumizi ya nishati safi ya kupikia. 

Ameeleza kuwa, Rais Dkt. Samia anathamini watanzania wote bila kujali hali zao na ndio maana ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia inagusa makundi yote ya Wananchi hivyo nao wana wajibu kumuunga mkono katika kuiletea Tanzania maendeleo.