Back to top

Rais Hussein Mwinyi amteua makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

08 November 2020
Share

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dakta Hussein Ali Mwinyi amendelea kuunda Serikali yake ambapo amemteua   aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba, Bwana Hemed Seleman Abdulla kuwa makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Uteuzi huo umetaganzwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mhe.Zubeir Ali Maulid, baada ya ku kamilisha zoezi la kuwaapisha wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ambapo kabla ya hapo wajumbe hao walipiga kura ya kumchagua spika mpya .

Akizumgumza na ITV Makamu wa Pili wa Rais mpya wa Zanzibar amesema ameshitushwa na uteuzi huo, lakini ameukubali kwa vile Rais amemuamini.