Rais wa Zanzibar Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameipongeza kamati ya maandalizi ya sherehe hizo na hasa kwa maonesho ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania kuonesha kuwa lina uwezo wa kuilinda nchi.
Ametoa kauli hiyo katika hotuba yake ya kilele cha maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwenye Uwanja wa New Amani Complex Mjini Unguja.
Rais Minyi pia amempongeza Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine, kwa kushiriki kwenye uzinduzi wa miradi mbalimbali kuelekea kilelele cha Mapinduzi ya Zanzibar.
Katika hotuba yake Rais MWINYI ameomba hotuba yake ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar hapo jana iliyojaa mambo mengi iendelee kutumika na vyombo vya habari.
Akizungumza katika sherehe hizo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, amesema sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar ndiyo mwanzo wa safari ya maendeleo.
Akitoa salaam zake Rais wa Uganda, Bwana Yoweri Museveni amewapongeza Wazanzibari kwa kuyalinda mapinduzi ambayo yalizaa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Naye Rais wa Rwanda, Bw.Paul Kagame amewatakia mafnikio Wazanzibari kutika kulinda mapinduzi ambayo yametimiza miaka sitini leo.
Sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais, Dkt.Philip Mpango, Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa na viongozi wengine wastaafu.