Back to top

RAIS MWINYI AZINDUA UWANJA MPYA WA AMAAN COMPLEX.

28 December 2023
Share

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali imedhamiria kujenga  uwanja mpya mwingine wa kisasa, ambao utatumika katika mashindano ya AFCON mwaka 2027.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo wakati akizindua rasmi Uwanja mpya wa Amaan Complex  Desemba 27, 2023, Mkoa wa Mjini Magharibi. 

Aidha, Rais Mwinyi ameeleza kuwa Serikali imelenga kujenga miundombinu ya michezo kila wilaya kwa viwanja vipya vya kisasa.

Vilevile Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Ujerumani kupitia shirika la maendeleo GIZ  imefunga mkataba wa makubaliano kwa ajili ya ujenzi wa viwanja vitano vya michezo midogomidogo ikiwemo mpira wa kikapu, mpira wa wavu , mpira wa mikono na mpira wa pete.