Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na Papa Francis mjini Vatican, na kuzungumza mambo kadhaa ikiwemo Elimu, Afya pamoja na kukuza amani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Holy See Press Office, mazungumzo ya viongozi hao ilienda vizuri huku wakiangazia mahusiano mema yaliyopo kati ya Tanzania na Holy See.
Aidha Baada ya Rais Samia kukutana na Baba Mtakatifu Francisko, Pia amekutana na Katibu wa Jimbo la Vatican, Kardinali Pietro Parolin, akifuatana na Katibu wa Vatican anayeshughulikia Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, Askofu mkuu Paul Richard Gallagher.