Back to top

Ripoti yabaini mapungufu katika maabara ya taifa ya afya ya jamii.

23 May 2020
Share

Kamati iliyoundwa kuchunguza mwenendo wa Mabara ya Taifa ya Afya ya Jamii inayohusika na upimaji na ukusanyaji wa sampuli za ugonjwa wa Corona, imebaini upungufu katika baadhi ya maeneo ukiwemo namna ya kuhifadhi sampuli za vitu mbalimbali ikiwemo damu na makohozi.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akikagua Maabara Mpya ya Taifa ya Afya ya Jamii yenye vifaa vya kisasa vyenye uwezo wa kupima sampuli elfu moa mia nane katika  saa ishirini na nne ambayo ujenzi wake umekamilika iliyopo Mabibo jijini Dar es salaam.

Amesema serikali imeanza kuufanyia kazi ushauri na mapendekezo  yaliyotolewa na kamati hiyo iliyoundwa, ukiwemo kuanza kuitumia.

Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Abel Makubi amesema wakati taifa linapokuwa katika siku tatu za kutoa shukurani kwa Mwenyezi Mungu, wananchi waendelee kuchukua tahadhari za kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona, kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalam wa afya, kwani kwa kufanya hivyo kutaongeza nguvu kwa serikali katika mapambano dhidi ya mambukizi mapya.