Back to top

Serikali yaanza mipango ya kupata ndege ya mizigo.

01 July 2019
Share

Serikali ya Tanzania imeanza mipango ya kupata ndege ya mizigo ili kusaidia upatikanaji wa masoko kwa urahisi kwa mazao ya wakulima ndani na nje ya nchi.

Mhandisi Isack Kamwelwe waziri wa Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano anayasema wakati akizundua rada ya kuongozea ndege katika kijiji cha Lumbila, kata ya Ruanda wilaya ya Mbozi mkoani Songwe.

Rada nyingine nne zinajengwa katika viwanja vya ndege vya kimataifa vya Julius Nyerere Dar es salaam, KIA mkoani Kilimanjaro, uwanja wa Mwanza na wa Songwe.