Back to top

Serikali yaondoa vikwazo vya uingizaji wa mbolea nchini.

04 July 2021
Share

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo nchini imetangaza rasmi kuondoa vikwazo vya uingizaji wa mbolea ili kupunguza uhaba wa mbolea na kuwaondolea mzigo wa gharama wakulima kutokana na utaratibu wa awali wa kutumia zabuni kutoleta ushindani.

Kauli hiyo imetolewa jijini Mwanza na Waziri wa Kilimo Prof.Adolf Mkenda ambapo amesema katika kuhakikisha mbolea zinaingia kwa ufanisi na kuwafikia wakulima kwa wakati wizara ipo tayari kufanya kazi bega kwa bega na  wanaoingiza mbolea kwa kufuata vibali vya udhiti wa ubora kutoka katika mamlaka ya udhiti wa ubora wa mbolea.

Kufuatia kuwepo kwa baadhi ya vikwazo vya uingizaji wa mbolea Prof.Mkenda anawatoa hofu waingizaji wapya na wazamani.

Tanzania inatajwa kuwa na uhitaji wa tani laki saba elfu 18 na 51 za mbolea kwa mwaka huku upatikanaji wake ukiwa ni asilimi 82.