Back to top

Shein akemea matumizi mabaya ya lugha.

19 December 2019
Share

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amekasirishwa na baadhi  ya taasisi na watu kutumia lugha ya kiswahili vibaya na kupoteza usahihi wake.

 Dk. Shein ametoa tahadhari hiyo katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na makamu wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd wakati akifungua kongamano la kimataifa la kiswahili liloandaliwa na Baraza la Kiswahili la Zanzibar ambapo amesema  kutumika lugha vibaya ni kwenda kinyume na utamaduni wa nchi na hivi sasa kiswahili ni lugha ya kiamtaifa.

 Dk.shein amewataka wataalam wa lugha kutumia fursa za kimataifa kwa vile lugha hiyo ni biashara kubwa na inatakiwa nchi nyingi.